Kocha mpya wa Bayern Munich, Pep Guardiola atamtumia kiungo nyota wa timu hiyo, Frank Ribéry kwa mfumo ule aliokuwa akimtumia Lionel Messi wakati akiwa Barcelona.
Guardiola ambaye ameanza kazi yake na Bayern Munich na kusema ana deni kubwa kutokana na mafanikio makubwa waliyoyapata msimu uliopita ndiye aliyesisitiza lazima Riberry aongeze mkataba.
Mfaransa huyo aliyejiunga na Bayern Munich mwaka 2007 akitokea Olympique de Marseille alishawishiwa na Guardiola kuongeza mkataba kwa kuwa anataka kumtumia kwa mfumo wa ‘False Nine’ ambao amekuwa akimtumia Messi.
False Nine maana yake namba tisa isiyo sahihi, iko hivi; kwa kuwa namba tisa hucheza kama mshambuliaji wa kati, Guardiola hutumia hiyo False Nine kwa namba tisa kucheza kama kiungo au kutoonekana kama ana namba uwanjani.
Tayari Guardiola ameeleza mpango wake wa kumtumia Riberry kama False Nine msimu ujao ili kufanya asumbue zaidi.
Kawaida False Nine, mchezaji lazima awe na kazi, uwezo wa kutoa pasi zitakazozaa mabao lakini pia kufunga tena kwa kupiga miguu yote miwili kwa uwezo ulio karibu sawa.
0 COMMENTS:
Post a Comment