ALCANTARA KUSHOTO... |
Kiungo mshambuliaji wa Barcelona, Thiago Alcántara amemalizana na mabingwa wa England, Manchester United.
Alcantara ambaye aliisaidia timu yakeya taifa ya Hispania kutwaa ubingwa wa Ulaya kwa vijana chini ya miaka 21 sasa ni mali ya United kwa kujibu wa mitandao mbalimbali ya Ulaya.
Kiungo huyo anatarajia kulipwa euro milioni 6 kwa kila msimu, kitu ambacho timu nyingine zilizokuwa zinamtaka zilishindwa kufanya.
Usajili wa kiungo huyo unaipa nguvu United kuimarisha safu yake ya kiungo ambayo ilionekana kutokuwa na nguvu na imeelezwa amekubali kuhama kwa kuwa angelazimika kuendelea kusubiri kwa kiungo cha Barcelona kina wakongwe lukuki kama Busquets, Xavi, Iniesta na Cesc.
0 COMMENTS:
Post a Comment