Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) limekataa kuwatambua mabondia watatu kati ya waliofungwa jela nchini Mauritius kutokana na kupatikana na hatia ya kukutwa na madawa ya kuletwa.
Kiongozi wa BFT, Makole Mashaga amesema bondia wanayemtambua kati ya hao ni PetroMtagwa tu wakati wengine hawawajui hata kidogo.
“Tumesikia mabondia waliofungwa ni wane, lakini sisi tunamtambua bondia mmoja tu. Wengine walipatikana kwa kutokuwa na hatia na wakarejea nchini na sasa wanaendelea na maisha yao.
“Sasa wakisema kuna mabondia mabondia wengine watatu, sisi hao hatuwatambui na hatujui ni akina nani,” alisema Mashaga.
0 COMMENTS:
Post a Comment