Kutua kwa Carlo Ancelotti
katika klabu ya Real Madrid maana yake ule mfumo wa Kocha Jose Mourinho utakuwa
umekufa.
Mourinho amekuwa akitumia
mifumo mbalimbali ikiwemo ile inayolazimisha timu kujilinda sana na
kushambuliajia kwa kushitukiza.
Karibu kila timu
aliyefundisha Muitaliano huyo amekuwa akitumia mfumo we 4-3-3 ambao asili yake
ni nchini Italia.
Mfano wakati akiwa AC
Milan alipata mafanikio makubwa akitumia mfumo huo na kubeba makombe lakini
baadaye akafanya hivyo baada ya kutua Chelsea ya England ambako pia alibeba
ubingwa.
Pamoja na hivyo, msimu
uliopita Ancelotti aliendelea kufanya vizuri akitumia 4-3-3 akiwa na PSG nchini
Ufaransa pia katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kutokana na mfumo wake
maana yake kuna baadhi ya wachezaji waliokuwa hawapati namba Real Madrid
watapata nafasi ya kucheza.








0 COMMENTS:
Post a Comment