Kipa Iker Casillas
amecheza mechi yake ya 800 akiwa mchezaji wa kulipwa.
Rekodi hiyo angweza
kuifikia miezi miwili au mitatu iliyopita lakini ilishindikana kwa kuwa kocha wa
zamani wa Real Madrid, Jose Mourinho aliamua kumuweka nje kwa kuwa walikuwa na
tofauti zao.
Casillas ametimiza rekodi
hiyo ya mechi 800 wakati akiichezea timu yake ya taifa katika mechi ya Kombe la
Mabara dhidi ya Japan.
Katika michuano hiyo
inayoendelea nchini Brazil, pamoja na kukaa muda mrefu nje ya uwanja, Casillas
alisema alijiona kama ndiyo anaanza kucheza soka la kulipwa.
“Nilijiona kama ndiyo
mpya, mambo yalikwenda tofauti kabisa. Lakini nashukuru kila kitu kimekwenda
vizuri na furaha yangu inaonekana wazi,” alisema.








0 COMMENTS:
Post a Comment