June 30, 2013




Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts ameonyesha kufurahishwa na uongozi wa klabu yake kumsajili kipa Deogratius Munish ‘Dida’.

Akizungumza kutoka nchini Uholanzi, Brandts alisema Dida kutoka Azam FC ni kati ya makipa waliokuwa wanamvutia sana.

 “Nimefurahi, naweza kusema uongozi umefanya kazi nzuri kwa kuwa Dida ndiye kipa niliyekuwa ninamtaka katika kikosi changu. Nilizungumza nao na kuwaeleza kama wataweza kumpata litakuwa ni jambo zuri sana,” alisema Brandts. 



Brandts anatarajia kuwasili nchini kesho usiku akitokea kwao Uholanzi ambako alikwenda kwa mapumziko baada ya Yanga kujitoa katika michuano ya Kagame kutokana na kuhofia usalama.

Hivi karibuni, Yanga iliamua kumrudisha kipa Yaw Berko lakini Brandts akawa mbogo kwa kuwa alionyesha kutokukubaliana na hali hiyo.
Hivyo Yanga wakaanza tena suala la kusaka kipa naye akapendekeza usajili wa Dida.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic