Mechi ya leo ya fainali ya Kombe la Mabara kati ya wenyeji Brazil imepewa jina la “Mechi ya wataalamu, dhidi ya wachawi”.
Nyota wa soka, Pele amesema Hispania inafaa kupewa jina la wataalamu kwa kuwa ina wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa kama vile Andrés Iniesta na Xavi na uchezaji wao ni gumzo.
Lakini Brazil ni timu ya wachawi, huku akimtolea mfano Neymar kwamba ana uwezo mkubwa wa kufanya kitu kinachoweza kushangaza wengi wakati wowote.
INAPIGWA HAPA MARACCANA |
Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu tayari ni gumzo pia nchini Tanzania ingawa wengi wamekuwa wakiona ugumu kwa kuwa itachezwa saa 7 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Brazil imeingia fainali baada ya kuichapa Uruguay kwa mabao 2-1 wakati Hispania iliitoa Italia kwa mbinde baada ya kumaliza mechi na mikwaju 7-6 ya penalty.
0 COMMENTS:
Post a Comment