June 29, 2013



 
Kipre (kulia) akiwa kazini...

Wachezaji wawili nyota wa Azam FC, mshambuliaji Kipre Tchetche na pacha wake Bolou watachelewa kujiunga na wenzao kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Msemaji wa Azam FC, Jaffar Idd amesema wachezaji hao wawili watabaki Ivory Coast kwa muda kwa ajili ya kumalizia masuala ya harusi.
 
Bolou (kushoto)...

“Bolou anafunga ndoa, hivyo lazima mwenzake awe pale kwa ajili ya kumsaidia na mara moja baada ya harusi, wataondoka kuja Dar kuungana na wenzao,” alisema Idd.

Kuhusiana na mazoezi, alisema: “Wachezaji wengine wameishaanza mazoezi tokea Juni 24, ila waliokuwa katika timu za taifa wenyewe walipewa likizo ya wiki moja.

“Baada ya hapo wataungana na wenzao na tutaendelea na maandalizi kama kawaida,” alisisitiza Idd.

Azam ilimaliza msimu ikiwa katika nafasi ya pili kwa mwaka wa pili mfululizo.

Uongozi wa timu hiyo umekuwa ukisisitiza kutaka kubeba ubingwa baada ya kikosi chao kukomaa tayari kwa mapambano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic