June 19, 2013


Luhende wa Yanga katika mechi dhidi ya Azam FC...


Na Saleh Ally
Kocha Kim Poulsen ameamua kumuita beki wa kushoto wa Yanga, David Luhende kuongeza nguvu katika kikosi chake.

Stars inatarajia kuingia kambini mwanzoni mwa mwezi ujao kujiandaa na mechi yake ya kwanza ya michuano ya Chan dhidi ya Uganda.

Poulsen ameamua kumuita beki huyo kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya mechi hizo mbili.


Chanzo cha habari cha uhakika kimeiambia Salehjembe kwamba Luhende atatangazwa ndani ya kesho na keshokutwa kwamba atakuwa kati ya wachezaji wa kikosi hicho.

Juhudi za kumpata Poulsen raia wa Denmark zilifanikiwa lakini alionyesha kutoa nje kiana.

“Suala la kutanga mchezaji kaitwa ni la msemaji wa TFF, hivyo unaweza kuwasiliana naye kama kuna kitu chochote.

“Lakini tuko kwenye majadiliano ya kuangalia kama tunaweza kuimarisha kikosi chetu kwa ajili ya michuano ya Chan dhidi ya Uganda kwa kuwa tunataka kwenda Afrika Kusini,” alisema Poulsen, dakika 15 zilizopita.

Lakini chanzo hicho kilisema hivi: “Nakuhakikishia ni uhakika na ndiyo ulikuwa mjadala wa leo, Luhende atatangazwa kati ya kesho na keshokutwa kwa kuwa Poulsen mwenyewe ndiye amemuita.”

Hivi karibuni, Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts kupitia Salehjembe alieleza masikitiko yake kuhusiana na kuitwa na kutoitwa kwa Luhende ili kuisaidia Taifa Stars kwa kuwa kiwango chake kilikuwa kizuri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic