June 30, 2013





Kocha Mkuu wa Man United, David Moyes na Wayne Rooney wamekutana kimyakimya na kumalizana.

Rooney na Moyes wamekutana mjini Manchester na kumaliza tofauti zao.
Kati ya kazi kubwa aliyokuwa anataka kuifanya Moyes mwanzo kabisa ilikuwa ni kukutana na Rooney.

Taarifa za ndani kutoka Man United zinaeleza baada ya wawili hao kukutana, mambo yamekwenda vizuri na Rooney ameonyesha hana tatizo na kocha huyo.



Rooney na Moyes waliwahi kufanya kazi pamoja wakiwa Everton na kocha huyo ndiye aliyempandisha Rooney katika kikosi cha kwanza na kufanikiwa kucheza Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza.

“Katika kikao, Rooney alisema wazi kwamba hana tatizo na Moyes pamoja na kwamba waliwahi kukwaruzana wakiwa pamoja Everton,” chanzo kiliambia gazeti la The Sun la Uingereza.

“Lakini alikuwa wazi kuhusiana na kukerwa kupita kiasi kuhusiana na suala la kuachwa katika mechi kubwa kama ile dhidi ya Real Madrid.

“Rooney alisisitiza hakufurahia kabisa kitendo hicho cha Ferguson ambaye aliendelea kumuacha nje katika mechi kadhaa muhimu.”

Tayari Barcelona ilionyesha nia ya kumnasa Rooney lakini Chelsea ilishatangaza hadi dau la pauni milioni 25.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic