Timu
ya Kilimanjaro FC ya Sweden, mchana huu inashuka dimbani mjini Stockholm
kukipiga na Blue Hill IF katika mechi ya kirafiki inayosubiriwa kwa hamu kubwa.
Kilimanjaro
FC inayoundwa na Watanzania wanaoishi nchini humo imekuwa tishio kwa timu
mbalimbali inazokutana nazo.
Asilimia
kubwa ya Watanzania wanaoishi nchini humo wamekifanya kikosi hicho kuwa moto wa
kuotea mbali.
Mmoja
wa viongozi wa Kilimanjaro FC, Nyupi Mwakikosa amesema mechi hiyo ni sehemu ya
kuimarisha kikosi lakini kuwapa mawakala kadhaa kuwaona wachezaji wao.
“Tunaendelea
kucheza mechi nyingi za kirafiki ili kuimarisha zaidi kikosi chetu kwa kuwa
tunaweza kushiriki ligi za juu kidogo msimu ujao.
“Lakini
tunawapa nafasi mawakala mbalimbali kuwaona wachezaji wetu hapa, huenda wengine
wakapata timu,” alisema Nyupi.
Raia
wengine kutoka katika nchi za Afrika nao wameunda vikosi vyao lakini
Kilimanjaro FC imekuwa ‘tatizo’ kwao kutokana na kutoa vipigo karibu kila
inapokutana nao.
0 COMMENTS:
Post a Comment