Kocha
wa zamani wa Simba, Patrick Liewig amesema anajisikia mpweke hasa unapofika
wakati wa jioni.
Liewig
raia wa Ufaransa amesema anatamani angekuwa kazini akijumuika na wachezaji wa
Simba ambao alikuwa na mipango mingi.
“Wakati
mwingine najikutaka nataka kutoa machozi, natamani kwenda mazoezini lakini
naona si sahihi kufanya hivyo.
“Natamani
kuwaona vijana wangu ambao wengi niliwaandaa na nilijua msimu mpya ningefanya
nao mambo mengine makubwa zaidi kwa kuwa msimu uliopita ndiyo tulikuwa tumeanza
kufanya kazi pamoja.
“Lakini
haitawezekana tena, haya ndiyo maisha ya mpira, hivyo nitakuwa nikiwasubiri
Simba wanilipe ili niondoke mapema. Najisikia vibaya kuendelea kukaa hapa,”
alisema.
Tayari
Simba imeshathibitisha kwamba kocha huyo atalipwa ndani ya siku chache kitita
cha dola 26,000.
Hata
hivyo, kumekuwa na mkanganyiko, kwani pamoja na Rage kukubali ni dola 26,000,
katibu wake Evodius Mtawala amesema kocha huyo anadai dola 20,000 tu na si
vinginevyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment