Iingawa imepita, lakini kati ya vivutio
vilivyojitokeza katika mechi kati ya Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast baada ya
kipa namba moja wa timu hiyo Boubacar Barry kumpa mtoto mmoja aliyekuwa
uwanjani pale glovu zake.
Kipa huyo anayekipiga katika timu ya
Lokeren ya Ubeligiji alitoka kama kawaida kwenda kupasha misuli na wachezaji
wenzake.
Baada ya takribani dakika 20 za kufanya
mazoezi ya kutosha Boubakar maarufu kama Copa alianza safari ya kurejea
vyumbani na wenzake.
Akiwa amefika nyuma ya benchi la Ivory
Coast alimuona mtoto huyo anayekadiriwa kuwa na miaka nane hadi kumi, mara moja
alielekea upande wake na kumrushia glovu zake mbili.
Dogo ambaye jina lake halikujulikana
mara moja naye alikuwa ‘shap’, aliinuka na kuzidaka glovu hizo lakini ajabu mtu
mwingine anayekadiriwa kuwa na miaka 25 hadi 30 aliinuka na kutaka kuzichukua
kwa madai yeye ndiye alimuita kipa huyo hadi akazirusha.
Lakini juhudi zake zilikwama baada ya
watu waliokuwa eneo hilo kutaka amuachie bwana mdogo huyo glovu zake hizo
zilizokuwa na jina la Copa.
Jamaa hakuwa na ujanja, pamoja na
kulaumu dogo huyo alibaki na glovu hizo na mwisho akaziinua kuashiria ushindi
na watu wakamshangilia kwa nguvu.
0 COMMENTS:
Post a Comment