Jamaa mwenyewe ni huyo mwenye traksuti nyeusi, angalia mkononi anavyochana hiyo karatasi huku akiendelea kusoma maneno, pia kama daktari, angalia alipokaa.. |
Mechi kati
ya Ivory Coast dhidi ya Taifa Stars ilikuwa na vituko vingi, si lahisi vikawa
simulizi ya siku moja kwa kuwa ilikuwa na upinzani mkubwa na kikosi cha wageni
kiliundwa na nyota wengi katika soka duniani.
Ivory Coast
pamoja na kuwa ugenini ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 na kufuta
matumaini ya Watanzania kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.
Pamoja na
uwezo waliounyesha Ivory Coast, kitu cha ajabu kabisa ni mmoja wa memba wa benchi
lao la ufundi kuonekana akifanya kazi zilizoonekana wazi kuwa ni za
kishirikina.
Kwa nini
mshirikina?
1. Kwanza mtu huyo ambaye mwanzo alitambulishwa kama
daktari wa timu, hakuwa akifanya kazi hizo na wengine ndiyo walikuwa ‘bize’.
Lakini ukifuatilia, utagundua hakuwa amekaa sehemu ambayo anaweza kukaa daktari
kama ambavyo madaktari wa kweli walipokuwa wamekaa.
2. Alionekana muda mwingi akifuatilia mchezo kuliko hata
wachezaji wenyewe huku akiwa ameshika karatasi mkononi halafu akawa anazungumza
kama mtu anayesali.
3. Baadaye aliendelea kusema maneno lakini safari hii
zile karatasi alizokuwa nazo mkononi alikuwa akizichana moja baada ya nyingine.
4. Kuonyesha alikuwa ni mtu wa kubandikwa kwenye benchi,
hakuwa hata na siti. Hivyo alilazimika kuibia siti za wachezaji na waliporudi,
alipiga makoti nyuma ya viti vya wachezaji na kuendelea na kazi yake.
5. Baada ya mechi, wakiwa vyumbani, wakati madaktari wa
timu wakiendelea kuwa ‘bize’ na wachezaji, yeye alikuwa busy akifunga vitu
vyake huku akiandika mambo kadhaa na baada ya hapo akakaa pembeni kimyaa.
unahushahidi au mastor ya town???? andika vitu vyenye mantiki
ReplyDelete