SSENKOOMI WAKATI AKIWA URA, AKIWANIA MPIRA NA MRWANDA ALIYEKUWA SIMBA |
Pamoja na kumpata na kumpata beki Samuel Ssenkoomi, Simba inaendelea kusaka beki mwingine wa kigeni.
Nchi ambazo Simba inaendelea na kumsaka beki huyo ni Kenya, Uganda, Rwanda na DR Congo.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza kwamba Msimbazi wanaonekana kutoridhishwa vya kutosha na kiwango cha beki huyo Mganda.
“Kweli tunaendelea kusaka beki ambaye ataweza kuwa na kiwango cha juu zaidi lakini wakati huo tukimba muda Ssenkoomi.
“Kwa kuwa tuna muda lakini hatutaki kubahatisha mambo, hivyo Samuel atapata muda na kama atapatikana beki mwingine naye atakuja kwa majaribio,” kilieleza chanzo.
Taarifa zinaeleza Simba imekuwa ikisaka mabeki katika nchi tatu na mmoja kati yao atasajiliwa na kucheza pamoja na Shomari Kapombe.
Tokea ametua nchini, Ssenkoomi ameonekana kutowaridhisha wengi wakiwemo mashabiki wa Simba na hasa kuhusiana na kimo chake.
Lakini bado hajapata muda wa kucheza kwa kuwa siku chache baada ya kutua nchini akaumia.
0 COMMENTS:
Post a Comment