Kocha Jose Mourinho amesaini mkataba
wa miaka minne ya kuifundisha Chelsea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chelsea, Ron
Gourlay amesema: “Ninayofuraha kubwa kumkaribisha Jose. Tunaamini ataendeleza
mbio zake za mafanikio, ni lengo letu kuipa mafanikio zaidi klabu hii, Jose ndiye
chaguo letu la kwanza na tuna muamini.
“Ameendelea kuwa kipenzi cha wengi
klabuni hapa, kila mtu anategemea makubwa kutoka kwake.”
Mourinho ametua na makocha wengine
wasaidizi Rui Faria, Silvino Louro na Jose Morais.
0 COMMENTS:
Post a Comment