KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amegusia
juu ya kumsajili mshambuliaji Wayne Rooney wa Manchester United.
Wenger ameamua kuweka wazi hisia zake
hizo kutokana na mchezaji huyo kutokuwa na dalili ya kuendelea kuichezea timu
hiyo, ambapo pia anawaniwa na Chelsea, Paris Saint-Germain na Bayern Munich.
Wenger amenukuliwa akisema: “Rooney ni
mchezaji mzuri kwa yeyote, nani ambaye hataki kuwa naye? Itategemea na kile
ambacho atakuwa anakihitaji lakini ikiwezekana tutamsajili.”
0 COMMENTS:
Post a Comment