Kamati ya Utendaji ya klabu
ya Simba inakutana kesho jioni kujadili masuala mbalimbali na kubwa ni
kuhusiana na usajili wao.
Katika suala la usajili,
kamati hiyo ya utendaji itajadili na kupata jibu sahihi kuhusiana na kipa Juma
Kaseja kwamba kama iendelee kubaki naye au la.
Chanzo cha ndani kutoka
ndani ya Simba kimeeleza Kaseja hakupata nafasi ya kufanya mazungumzo na
uongozi wa Simba baada ya kutaka kukutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili,
Zacharia Hanspope na si mtu mwingine.
“Ukweli kuhusiana na suala
la Kaseja ni kwamba bado hatujakuwa na jibu la uhakika na lazima kamati ya
utendaji ikutane na kupata jibu la mwisho kuhusiana na hilo.
“Hivyo kesho jioni tutakuwa
na jibu na tumeelezwa Kaseja yuko kwao Kigoma ana masuala ya kifamilia. Lakini sisi
tutakaa na kujua.
“Awali alikuwa azungumze na
Mzee Kinesi lakini yeye akasisitiza lazima azungumze na Hans Pope yeye
mwenyewe. Tunaendelea kusubiri kuhusiana na hilo halafu tutajua baadaye ni
vipi.
“Mwanzo pia kulikuwa na
mazungumzo na Kaseja lakini akasema dau kubwa, hivyo naweza kusema bado hakuna
jibu sahihi kuhusiana na kubaki au kuachwa na ukiangalia muda wa usajili bado
kabisa, unaweza kusema sasa ndiyo usajili umefunguliwa,” kilieleza chanzo cha
uhakika.
Mara kadhaa kumekuwa na
taarifa kwenye vyombo vya habari kwamba Simba imeachana na Kaseja na anatua
Azam FC, lakini mara zote viongozi wa Simba wamekuwa akitaka kuwepo kwa sbira.
0 COMMENTS:
Post a Comment