June 26, 2013



Kocha mpya wa Manchester United, David Moyes atazungumza na mshambuliaji wake Wayne Rooney na kumtaka abaki Old Trafford.
Mskochi huyo mwenye miaka 50, atazungumza na Rooney baada ya kurejea kutoka nchini Marekani.

Uamuzi huo wa Moyes umeelezwa na rafiki yake wa karibu kwamba anataka Rooney abaki badala ya kuondoka kama ambavyo imekuwa ikielezwa.

Rooney ,27, ameonekana kuwa anataka kuondoka Man United kwa kuwa uhusiano wake na aliyekuwa Kocha Mkuu, Alex Ferguson ulidorora.


Tayari Chelsea na Arsenal zilikuwa zimeanza kuonyesha nia ya kumchukua kama ataamua kuondoka.

Lakini Barcelona pia walionyesha nia ya kutaka kumpata Rooney na kuongeza nguvu katika safu yao ya ushambuliaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic