June 26, 2013





Cristiano Ronaldo bado hajamaliza hamu yake ya kujaribu kurejea katika klabu yake ya zamani ya Manchester United.

Taarifa zinaeleza kuwa atakutana na viongozi wa Manchester United ndani ya siku tatu zijazo na kujadili nao tena kama inawezekana kurejea au la.
Hata hivyo, tayari Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ameishawahakikishia wanachama na mashabiki wake kwa mshambuliaji huyo mwenye thamani ya pauni milioni 80 ataendelea kubaki Bernabeu.


Gazeti la El Pais la Hispania limeeleza Mreno huyo atazungumza na viongozi hao wa Man United kabla ya kujiunga na Real Madrid kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Lakini kwa kuwa Fifa inakataza klabu kuzungumza na mchezaji yoyote mwenye mkataba unaozidi miezi sita, kila upande umeukana mkutano huo ambao gazeti hilo limesisitiza utafanyika.

Ronaldo alijiunga Real Madrid akitokea Man United ambako alijenga jina chini ya Kocha Alex Ferguson ambaye amestaafu baada ya kwisha kwa msimu uliopita.

Nyongeza:

  Manchester United stats
League - Apps: 196 Goals: 84
Cup - Apps: 38 Goals: 17
Europe - Apps: 55 Goals 16
Real Madrid stats
League - Apps: 135 Goals 146
Cup - Apps: 20 Goals: 17
Europe -  Apps: 40 Goals: 35

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic