Kocha wa Yanga, Ernie Brandts
anatarajia kurejea kwao Uholanzi kwa muda.
Brandts atarejea Uholanzi, taarifa hizo
zimepatikana siku moja tu baada ya Yanga kutangaza kujitoa katika michuano ya
Kombe la Kagame.
Yanga imetangaza kujitoa katika michuano
ya Kagame iliyopangwa kufanyika nchini Sudan kwa sababu za kiusalama.
“Kweli kocha atarudi nyumbani kwa kuwa
hakuna kitu cha kufanya kwa kipindi hiki na tayari wachezaji wamepumzishwa kwa
wiki mbili sasa.
“Awali ilikuwa ni kwa ajili ya
maandalizi ya Kombe la Kagame, lakini tumejitoa kama ulivyosikia na hakuna
sababu ya kocha kuendelea kuwa hapa kwa sasa.
“Atasafiri na baada ya kurejea ataanza
maandalizi kwa ajili ya ligi na kambi tutaiweka rasmi,” kilieleza chanzo ndani
ya Yanga.
Brandts alikuwa mapumzikoni Uholanzi na
Hispania kabla ya kurejea nchini tayari kwa kazi na alishaanza maandalizi kabla
ya Yanga kujitoa kwa sababu za kiusalama.
0 COMMENTS:
Post a Comment