Kikosi cha timu ya
Simba, kesho kitashuka uwanjani kwa mara ya pili kucheza mchezo wa kirafiki wa
kujipima nguvu dhidi ya Golden Bush.
Huo utakuwa mchezo
wa pili kwa Simba inayonolewa na kocha mkongwe Abdallah Kibadeni ambapo awali
kikosi hicho kilicheza mchezo wake wa kwanza wa kujipima nguvu dhidi ya Friend
Rangers ya Manzese, mchezo ambao ulichezwa katika Uwanja wa Kinesi uliopo
Ubingo jijini Dar ukimalizika kwa sare
tasa.
Akizungumza jijini
Dar, Kibadeni maarufu kwa jina la King amesema mchezo huo utakaopigwa katika
uwanja wa Kinesi dhidi ya vijana hao wa Golden Bush inayonolewa na nyota wa
zamani wa Simba Madaraka SelemanI itakuwa ni mechi nzuri ya kukipima kikosi
chake ambacho kipo katika mazoeziu makali kwa muda wa wiki mbili sasa.
“Kwasasa nataka
kwanza kucheza michezo na timu ndogondogo kwanza ili niweze kuangalia jinsi
vijana wangiu wanavyoelewa yale ninayowafundisha.
“Nafikiri kitakuwa
kipimo kizuri kwao na baada ya hapo nitajua nini cha kufanya ili tuendelee
kuijenga Simba imara,” alisema Kibadeni ambaye ni nyota wa zamani wa kikosi
hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment