June 23, 2013

SURE BOY AKIPOKEA TUZO KUTOKA KWA KATIBU MKUU TFF, ANGETILE OSIAH

Nyota imezidi kung’aa kwa kiungo wa Simba, Amri Kiemba baada ya juzi kufanikiwa kutangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita.

Kiemba alipata tuzo hiyo katika hafla fupi iliyofanyika juzi usiku katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar. Hafla hiyo ya kutangaza washindi wa tuzo mbalimbali za ligi kuu msimu uliopita, iliandaliwa na Chama cha Wachezaji wa Soka Tanzania (Sputanza).
 
MAXIME AKIPOKEA TUZO YA KOCHA BORA
Kiungo huyo aliwashinda nyota mbalimbali wakiwemo Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu (Yanga), Kipre Tchetche (Azam FC) na Paul Nonga (JKT Oljoro).
 
SKYLIGHT BAND WAKIKAMUA..


Tuzo ya kocha bora iliangukia kwa Mecky Maxime wa Mtibwa Sugar ambapo beki huyo wa zamani wa timu hiyo na kikosi cha Taifa Stars, aliwashinda Charles Boniface Mkwasa (Ruvu Shooting), Abdallah Kibadeni (Kagera Sugar - sasa Simba) na Jumanne Charles (Prisons).
 
KHATIM NAHEKA 'NTU WA NGUVU' WA CHAMPIONI NA MTU WANGU WA NGUVU MILLARD AYO WA CLOUDS FM WALIKUWA NDANI YA NYUMBA..
Nyota mwingine aliyeibuka kidedea ni kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ aliyetwaa tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi akiwaacha Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Twaha Shekue (Coastal Union) na Shomari Kapombe (Simba).
 
MGENI RASMI, MAKAMU WA KWANZA WA RAIS TFF, ATHUMANI NYAMLANI NA WADHAMINI PEPSI..
Pia kipa Hussein Sharif ‘Casillas’ (Mtibwa Sugar), alifanikiwa kuwabwaga makipa wengine wawili katika tuzo ya kipa bora ambapo aliwashinda Juma Kaseja (Simba) na Mwadin Ally (Azam FC).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic