Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi ameanza kulipa kodi aliyokwepa na imeelezwa tayari ametoa euro milioni 10.
Ingawa Messi alisema hana kosa na alilipa kodi, lakini jarida la Vanguardia limeeleza Muargentina huyo amelipa kiasi hicho cha fedha ambacho kinahusisha kodi ya miaka miwili ya 2010 na 2011.
Messi anatuhumiwa kukwepa kodi kuanzia mwaka 2007 hadi 2011 ambazo alizikwepa wakati alipofanya biashara kubwa ya kuuza haki ya picha zake.
Suala la Messi na baba yake mzazi Jorge Messi kukwepa kodi limekuwa gumzo na tayari imeelezwa watapanda kizimbani Septemba mwaka huu.
Taarifa nyingine kutoka katika jarida hilo zimeeleza Messi yuko katika mazungumzo na wahusika wa masuala ya kodi ili ikiwezekana alipe pia kodi za miaka ya 2007,2008 na 2009 ambazo hakuwa amelipa.
Hata hivyo inaonekana suala hilo limekuwa likifanywa siri kubwa ili kuepuka kuonekana atakuwa amependelewa.
0 COMMENTS:
Post a Comment