Messi akiwa nchini Senegal... |
Kwa mara ya kwanza mshambuliaji nyota wa FC Barcelona, Leo Messi amemzungumzia mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Neymar.
Neymar raia wa Brazil amekuwa gumzo kubwa tokea atue Barcelona huku wengi wakiamini ni kosa kwake kujiunga na Messi akiwa timu hiyo.
Messi akiwa nchini Senegal jana ambako alikwenda kwa ajili ya kuhimiza kampeni kuhusu kupambana na ugonjwa hatari wa malaria.
Alipoulizwa swali kuhusiana na Neymar kwamba kuna hofu ya kuwa hawataelewa wakiwa katika vyumba vya kubadilishia nguo, alisema:
“Neymar ni mchezaji bora kabisa, ninaamini tutashirikiana kuifanya Barcelona kuwa tishio zaidi. Pia ninaamini ataifantia Barcelona ambayo anayafanya sasa kwa Brazil.”
Messi alikuwa hajawahi kuzungumzia suala hilo wakati Neymar mara kadhaa ameishalizungumzia ikiwa ni pamoja na kuelezea atakavyomsaidia Messi kuendelea kubaki mchezaji bora wa dunia.
0 COMMENTS:
Post a Comment