June 29, 2013





Mshambuliaji wa Brazil, Neymar amesema wana kikosi imara cha kuizuia Hispania kutwaa ubingwa wa Mabara na kuweka historia.

Iwapo Hispania itaishinda Brazil katika mechi ya fainali ya Kombe la Mabara Jumapili kwenye Uwanja wa Maraccana maana yake itakuwa imeweka rekodi ya kuchukua makombe yote makubwa yaani Kombe la Dunia, Kombe la Ulaya na KOmbe la Mabara.

Nelly amewaambia waandishi wa habari mjini Rio De Janeiro kwamba wana kila sababu ya kuizuia Hispania ambayo inaonyesha katika historia haijawahi kukutana na Brazil kwa miaka 27 iliyopita.



Brazil imeingia fainali kwa kuichapa Uruguay kwa mabao 2-0 wakati Hispania imeing’oa Italia kwa tabu baada ya kuichapa kwa mikwaju ya penalti 7-6.

Neymar atakutana na wachezaji ambao wanakuwa timu mmoja msimu ujao na baadhi yao ni Xavi, Iniesta, Pedro na huenda akachukuana muda mwingi na beki Pique ambaye pia watakuwa naye Barcelona.

1 COMMENTS:

  1. Neymar est connu pour ses dribbles, ses finitions et ses capacités avec les deux pieds

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic