Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadicky ametoa mpya leo alipombandika jina jipya mshamnbuliaji wa Ivory Coast.
Sadicky alikuwa akizungumzia mchezo wa
kesho kati ya Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast kuwania kucheza Kombe la Dunia
na kusema wachezaji wa Stars hawapaswi kuwa waoga na kuhofia majina makubwa ya
wageni wao.
Alisema huku akiyataja moja ya majina
hayo kuwa ni Kalalu akimaanisha Kalou, kwamba hawana haja ya kuwahofia hata
kidogo.
Kutokana na Sadicky kukosea hayo majina,
waandishi na wengine waliokuwa katika eneo hilo waliangua kicheko na
kumrekebisha kiongozi huyo.
Hata hivyo, mkuu huyo wa mkoa
aliwashauri Stars kupambana bila ya woga kidogo na kusema hata kama ni ustaa,
wachezaji wa Stars nao ni mastaa pia hivyo wapambane na kuwamaliza vilivyo
Ivory Coast.
0 COMMENTS:
Post a Comment