June 14, 2013



 Mambo yamebadilika baada ya serikali ya Tanzania kupata barua kutoka serikali ya Sudan ikisema Simba, Yanga na Falcon zitapewa ulinzi wa uhakika.

Serikali ya Sudan imeiambia ya Tanzania kwa itahakikisha wachezaji, viongozi na mashabiki watakuwa salama nchini humo katika kushiriki michuano ya Kagame.

Tayari timu za Tanzania zilishatangaza kujitoa na Cecafa ikaanza kuzialika timu nyingine kuziba mapengo hayo.

Timu ya Tusker ya Kenya pia ilitangaza jana mchana kujitoa katika michuano hiyo ya Kagame ambayo ingepigwa katika miji ya Sudan ikiwemo Darfur ambayo inatawaliwa na machafuko.


Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla amethibitisha wao kupata barua hiyo kutoka Sudan.

Hata hivyo Makalla amesisitiza Simba, Yanga na Falcon wao ndiyo wataamua kama wanataka kwenda au la.

Hofu ya timu zote lilikuwa ni suala la usalama hasa katika mji huo wa Darfur ambao unajulikana kutokana na machafuko ya vita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic