June 30, 2013





Wasomaji wa gazeti la The Sun la Uingereza wamempa nafasi ya kwanza Kocha Mkuu wa Chelsea, Jose Mourinho kuwa atatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England akiwa na Chelsea.

Katika kura zilizopigwa kupitia gazeti hilo maarufu, wasomaji hao wametoa asilimia 52 za Mourinho kutwaa ubingwa wa England msimu ujao.

Wakati wamempa nafasi ya pili David Moyes wa Manchester United kwa kuchukua asilimia  28 za kutwaa ubingwa huo ambao sasa unashikiliwa na timu yake aliyoichukua kutoka kwa Alex Ferguson aliyestaafu.



Nafasi ya tatu imepelekwa kwa Manuel Pellegrini wa Manchester City aliyepewa asilimia 15 tu za kutwaa ubingwa.

Makocha hao wamekuwa gumzo na hasa baada ya Mourinho na Pellegrini kurejea katika Ligi Kuu England huku Moyes akiwa amechukua nafasi ya Ferguson aliyekuwa kocha bora zaidi katika ligi hiyo tokea ianzishwe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic