Kiemba akiwa na Ngassa wakati akiwa Simba... |
Kiungo wa Simba, Amri Kemba amepishana na mamilioni
kutoka kwenye moja ya klabu za nchini Ureno, lakini amepata nafasi nyingine ya
kufanya kazi na Waisrael.
Simba walipata ofa kutoka Ureno juu ya mchezaji huyo
lakini ikaweka dili hilo pembeni kwa kuwa walikuwa kwenye mazungumzo na Klabu
ya Raja Casablanca ya Morocco, ambayo pia ilikuwa ikimhitaji mchezaji huyo.
Zakaria Hans Pope ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba ameliambia Championi Ijumaa kuwa klabu yake imepokea ofa
kutoka kwa klabu moja kubwa ya nchini Israel inayomuhitaji Kiemba.
Alisema klabu hiyo ambayo hakutaka kuitaja jina lake
inamhitaji Kiemba na wametoa ofa kwa dola 200,000 (Sh milioni 320), ingawa
Simba imesema bei ya mchezaji huyo ni dola 400,000 (Sh milioni 640).
“Waisraeli wanaonyesha nia ya kumuhitaji sana kutokana
na kila mara wamekuwa wakitutumia barua pepe wakitaka tuwajibu juu ya hatua
tuliyofikia.
“Tunahitaji fedha lakini hatutaki kufanya mambo
kihuni, tunasubiri kwanza Raja Casablanca tuwasikie wamefikia wapi ila kwa hao
Waisrael wakishuka kwenye dau kidogo kama dola 300,00 au 250,000 tutakubali,”
alisema Hans Pope.
SOURCE:
CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment