Na Mwandishi Wetu, Mwanza
WAKATI Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) likiwa limetoa dola
500,000 kwa ajili ya kuweka nyasi bandia kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini
Mwanza, zipo dalili mpango huo kukwama.
Fedha hizo zimehifadhiwa mjini Gaborone nchini Botswana kwenye ofisi
za maendeleo ya Fifa, ambapo Halmashauri ya Jiji la Mwanza ilitakiwa kuchangia dola
118,000 ili kufikisha Dola 618,000 za mradi huo.
Hata hivyo uchunguzi umebaini kuwa kuna mpango wa uwanja huo kutumika
kwa ajili ya miradi mingine na ndiyo maana mchakato wa kuweka nyasi umekuwa
ukisuasua.
Akizungumza kuhusiana na kuwapo kwa mapendekezo hayo, Mwenyekiti wa
Chama cha Soka Mwanza (MZFA), Jackson Songora alisema: “Sina taarifa za
mapendekezo hayo, ninachofahamu walituandikia barua ya kuwa wabia katika mpango
huo pamoja na mfuko wa NSSF.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Tito Mahinya alipoulizwa kuhusiana na
mapendekezo hayo kupitia ujumbe mfupi wa simu alijibu kwa ufupi: “Hakuna kitu
kama hicho.”
SOURCE:
CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment