Pele akiwa na Neymar na Messi.. |
Gwiji la soka
duniani, Pele amesema alikuwa kati ya watu waliomzuia Neymar kwenda kucheza
soka nchini England.
Pele amesema anaamini kwa Neymar kwenda
Hispania ni wazo zuri kuliko England.
Katika mahojiano na redio moja nchini
Brazil, Pele alisema alimuambia Neymar asiende England baada ya kumueleza kuna
timu zinamuhitaji.
„Ingekuwa tatizo kwake kutoka Brazil na
kwenda kucheza katika ligi wanayotumia nguvu nyingi. Ingemsumbua, hivyo
nikamshauri asiende,“ alisema Pele.
Neymar amejiunga na Barcelona na tayari
imeishakuwa gumzo kuhusiana na atakavyoshirikiana na mkali wa timu hiyo, Lionel
Messi.
Lakini yeye Neymar amesema atamsaidia
Messi kuendelea kuwa mchezaji bora wa dunia, kitu ambacho wengi wanaona
haitakuwa sahihi.
0 COMMENTS:
Post a Comment