Mshambuliaji Wayne Rooney wa Man
United, ametinga katika shoo ya mwanadada Rihanna akiwa amenyoa katika staili
mpya.
Katika shoo hiyo iliyofanyika kwenye
Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester, Rooney alitinga ukumbini hapo akiwa
na mkewe Coleen na kusababisha awe kivutio kikubwa.
Pamoja na shoo hiyo, lakini siku hiyio
ilikuwa muhimu zaidi kwa Rooney na mkewe
Coleen ambao walikuwa wakitimiza miaka mitano ya ndoa yao.
Miaka kadhaa iliyopita, Rooney
alilazimika kutumia mamilioni ya fedha kufuta kipara lakini safari hii
alionekana akiwa ampunguza nywele zote na kuonekana kama upara tena.
Rooney
anahusishwa na kuondoka Man United na timu ambazo tayari zimeonyesha nia ya
kutaka kumsajili ni Chelsea, Arsenal na Paris St Germain ya Ufaransa.
0 COMMENTS:
Post a Comment