Mshambuliaji Luis Suarez wa Liverpool ameonyesha kwa mara nyingine kwamba
anataka kuondoka Anfield.
Kama hiyo haitoshi, Suarez amesisitiza anataka kucheza timu moja na Cristiano Ronaldo.
Kauli hiyo ya Suarez, maana yake anataka kuondoka Liverpool na kutua Real
Madrid ambayo imeonyesha nia ya kutaka kumchukua.
Pamoja na kauli hiyo, Suarez amekuwa akilaumu vyombo vya habari vya England
kumyima raha kwa kumuandama mara kwa mara.
Wakati vyombo hivyo vya habari vimekuwa vikimuelezea kama mchezaji
asiyejitambua kutokana na kufanya vituko vingi vya kitoto.
0 COMMENTS:
Post a Comment