Kocha mpya wa Chelsea, Jose Mourinho amesema yuko tayari kufanya kazi na
mshambuliaji Wayne Rooney.
Mourinho amesema Rooney ni kati ya wachezaji wanaomvutia na milango iko wazi
kama atakuwa tayari kufanya naye kazi Stamford Bridge maarufu kama darajani.
Rooney amekuwa hana raha siku chache baada ya Ferguson kustaafu soka kwa
kuwa walikuwa wamelumbana.
Lakini kutua kwa David Moyes ambaye ni kocha wake wa kwanza akiwa Everton
pia kunaonyesha hatakuwa na furaha kubaki Man United kwa kuwa waliwahi
kulumbana wakati wakiwa wote.
Hata hivyo, Chelsea iko katika vita ya kuhakikisha inamnasa mshambuliaji
Edinson Cavani wa Lazio.
Rooney ni mzaliwa wa Liverpool ambako alichupukia akicheza soka ambako
alijiunga na timu ya watoto ya Everton baada ya baba yake kukataa asichezee
Liverpool.
0 COMMENTS:
Post a Comment