July 18, 2013



Klabu ya Chelsea imetakiwa kuwarudishia fedha mashabiki waliotozwa fedha za ziada katika ziara yao Jakarta nchini Indonesia.

Mashabiki hao walitozwa pauni 1,500 (zaidi ya Sh milioni 3.7) ili kupata nafasi ya kukutana na nyota wa kikosi cha Chelsea wakati kikiwa jijini Jakarta, sasa Chelsea wanatakiwa kuwalipa fedha zao.

Kama hiyo haitoshi, Chelsea imetakiwa pia kuwalipa mashabiki wengine waliotozwa pauni 330 (karibu Sh 500,000) ili kupata nafasi ya kuhudhuria mazoezi ya hiyo pia warudishiwe haraka.

 

Uamuzi huo wa Chelsea umetokana na waandaaji kufanya mambo bila ya kuwataarifu au kuwapa ratiba kuhusiana na watu hao.

Baada ya timu kutua, kwa kuwa msafara wa Chelsea haukupewa taarifa mapema na kuamua kuhusiana na hilo, ukakataza watu kuwa karibu na wachezaji wao au mashabiki kuingia mazoezini. Lakini uongozi wa Chelsea umesisitiza haukutaarifiwa lolote kuhusiana na hilo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic