![]() |
| OGBU (KULIA) AKIWA MAZOEZINI NA YANGA... |
Mshambuliaji mpya wa Yanga, Brendan Ogbu kutoka Nigeria ameanza vibaya baada ya kuumia.
Ogbu ameumia siku ya pili tu ya mazoezi akiwa na Yanga kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Mabibo jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji huyo mwenye kasi aliumia wakati akiwa mazoezini na kulazimika kutoka nje ambako alipewa matibabu kwa zaidi ya dakika 15.
Baadaye alirejea uwanjani, hata hivyo aliendelea kuchechemea lakini akafanikiwa kufanya mazoezi.
Mshambuliaji huyo alisema kwamba alikuwa akisikia maumivu makali katika sehemu ya kifundo cha mguu hata baada ya mazoezi hayo.
Ogbu alianza mazoezi na Yanga jana, leo alikuwa acheze mechi ya kirafiki dhidi ya 3 Pillars iliyoelezwa inatokea Nigeria, lakini baadaye ikagundulika timu hiyo ni ‘bagumashi’, mechi ikaahirishwa.
Kuhusiana na kesho, Ogbu atalazimika kusikilizia hali yake na baada ya hapo atajua kama ataendelea na mazoezi au atapumzika.
Hata hivyo, anategemewa kucheza mechi ya Jumapili wakati Yanga itakapoivaa URA ya Uganda kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Obgbu yuko Yanga kufanyiwa majaribio, mara ya mwisho alikuwa anaichezea Heartland ya Nigeria.








0 COMMENTS:
Post a Comment