![]() |
| CISSE |
Mshambuliaji Papiss Cisse amegoma kufanya mazoezi na wenzake katika kikosi cha Newcastle kutokana na udhamini ilionao klabu hiyo.
![]() |
| BEN ARFA |
Newcastle ina udhamini wa kampuni ya mikopo ya Wonga ambayo imeilipa klabu hiyo pauni milioni 24.
Mshambuliaji huyo raia wa Senegal ni mwislamu na amekuwa imani yake haimruhusu kukubali kazi za Wonga ambayo inakopesha na kuchukua riba kwa wanaorudisha mikopo.
Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Newcastle ukiwa unaendelea kuangalia utalifanyiaje kazi suala hilo, umekubali Cisse aendelee na mazoezi akiwa gym.
Lakini mchezaji mwingine ambaye pia imani yake ni dini ya islam, Hatem Ben Arfa, yeye alionekana akiendelea na mazoezi huku akiwa amevaa jezi yenye logo ya Wonga.









0 COMMENTS:
Post a Comment