Mshambuliaji mpya wa Simba, Hamis Tambwe ameondoka
kurejea kwao Burundi ikiwa ni siku moja tu baada ya kusaini mkataba wa miaka
miwili Msimbazi.
Tambwe amerejea kwao kumaliza majukumu na atacheza
mechi mbili muhimu, moja dhidi ya Sudan kuwania kucheza Chan na ya pili akiwa
na timu yake ya Vital’O.
Mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili
kuichezea Simba, tayari akiwa ni mfungaji bora wa michuano ya Kagame
iliyofanyika nchini Suda.
Lakini Tambwe pia ni mfungaji bora wa Ligi Kuu ya
Burundi na alifunga mabao 18 yaliyompa nafasi hiyo. Msimu mmoja kabla alikuwa
mfungaji bora namba mbili baada ya kufunga mabao 16.








0 COMMENTS:
Post a Comment