July 5, 2013




Mkali namba moja wa mchezo wa tenisi duniani, Novak Djokovic amezima ndito za Juan Martin Del Potro na kutinga fainali ya michuano ya Wimbledon.


Katika nusu fainali hiyo ya kukata na shoka, upinzani ulikuwa mkali kupindukia na kusababisha mchezo huo uchukue saa nne na dakika 43 watu wakiendelea kushuhudia.

Djokovic raia wa Serbia alichukua alishinda kwa seti 7-5, 4-6, 7-6, 6-7, 6-3  na sasa anasubiri mshindi kati ya Waingereza Andy Murray  na  Jerzy Janowicz ambao wako uwanjani sasa wanaonyeshana kazi.

Tayari Murray anaongoza kwa seti mbili kwa moja, fainali hiyo itapigwa keshokutwa Jumapili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic