July 5, 2013



Kocha wa Man United, David Moyes amesema mshambuliaji wake Wayne Rooney, hatauzwa.

 Moyes amesema maneno hayo katika mkutano wake wa kwanza kwenye Uwanja wa Old Trafford, ukiwa ni wa kwanza tokea alipotangazwa kuchukua nafasi ya Alex Ferguson.


Moyes amewaambia waandishi kwamba Rooney ambaye alimuambia Ferguson mwishoni mwa msimu uliopita kwamba anataka kuondoka kwamba amebadili uamuzi.

“Wayne hatauzwa, ataendelea kuwa mchezaji wa Manchester United, tumezungumza mara kadhaa na tumekubaliana kufanya kazi pamoja,” alisema.

Hata hivyo bado kauli ya Rooney mwenyewe kwamba kama atabaki au la ndiyo inayosubiriwa kwa kuwa Moyes hakuweka wazi kama Rooney ameonyesha kuwa na furaha kuendelea kubaki United.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic