![]() |
| ROONEY WAKATI AKIWASILI ENGLAND, LEO... |
Manchester United imerudisha nyumbani England mshambuliaji wake Wayne Rooney kutokana na kuumia nyama za paja.
Pamoja na hivyo, Kocha wake David Moyes amemvaa Jose Mourinho na kusisitiza kuwa mshambuliaji huyo hauzwi.
![]() |
| MOYES |
Rooney alisafiri na Man United hadi Thailand kwa ziara ya bara la Asia, lakini amerudishwa leo nyumbani na Moyes amesema walikuwa wakijua kuhusiana na nyama hizo za paja lakini akamuonya Mourinho.
Mourinho amekuwa akisisitiza kuwa anavutiwa na uwezo wa Rooney na angefurahi kuungana naye Chelsea ambako ametua akitokea Real Madrid.
![]() |
| MOURINHO |
“Kurudia si kitu kizuri, lakini nalazimika kufanya hivi huenda nikaeleweka zaidi. Rooney hauzwi, ni mchezaji wa Manchester United na itabaki kuwa hivi.
“Jose anapaswa kuelewa kuhusiana na hili na ikiwezekana akaachana na kumzungumzia,” alisema na kunukuliwa na moja ya mitandao maarufu ya Hispania lakini kabla alifanya hivyo katika mtandao wa Uingereza wa Dailymail.










0 COMMENTS:
Post a Comment