Imebainika kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola alifanya kila juhudi kuhakikisha anamsajili mshambuliaji nyota Neymar.
Guardiola alitaka Neymar ajiunge na Bayern Munich na kufanya naye kazi badala ya kwenda Barcelona.
Kocha huyo mpya wa Bayern Munich, alifanya zoezi hilo kimyakimya na kukutana na baba mzazi wa Neymar na kumshawishi mwanaye akafanye kazi Ujerumani.
Guardiola alimueleza baba Neymar kwamba ingekuwa vigumu kwa kocha wa Barca, Tito Vilanova kuwatumia vizuri Messi na Neymar.
Makamu wa Rais wa Santos iliyomlea Neymar aitwaye, Odilio Rodrigues ndiyo ametoa siri kuhusiana na sakata hilo.
Rodrigues amesema kama si Neymar mwenyewe kuchagua Barcelona, basi angeweza kujiunga na Guardiola na kuichezea Bayern Munich.
Timu nyingine zilizokuwa zikimuwania waziwazi ni Real Madrid na AC Milan, lakini Barcelona ndiyo ikafanikiwa kumtwaa.








0 COMMENTS:
Post a Comment