Kocha José Mourinho wa Chelsea atarejea na kujiunga na timu yake ya zamani ya Inter Milan.
Taarifa zimeeleza Mourinho atajiunga na Inter kama atamaliza mkataba wake Chelsea, lakini bado itategemea kama atadumu hadi mwisho.
Gazeti la 'La Stampa' limesema Mourinho amezungumza na mmiliki wa Inter Milan, Masimo Moratti na kukubaliana yake kuhusiana na hilo
Tayari Mourinho amejiunga na Chelsea ambayo aliwahi kuifundisha na baada ya kuondoka alipumzika kabla ya kuibukia Inter Milan.
Kabla ya kutua Chelsea, kulikuwa na taarifa Mourinho angerejea Inter Milan lakini haikuwa hivyo na badala yake akatua jijini London.
0 COMMENTS:
Post a Comment