Mkutano wa wanachama wa klabu ya Simba
umefanyika leo na kumalizika kwa vituko kibao.
Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa
Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Katika moja ya vituko ni Mwenyekiti
Ismail Aden Rage kutaka kumtoa mmoja wa wanachama Bi Hindu ambaye ni msanii
maarufu wa uigizaji.
Rage aliinuka kutoka meza kuu na kutaka
kumtoa Bi Hindu baada ya kuwa akiitikia kwa nguvu.
Mwenyekiti huyo alifika eneo alilokaa Bi
Hindu na kutaka kumtoa kwa nguvu, huku akiita askari.
Lakini Bi Hindu akagoma na wanachama
wengine wakamsaidia hivyo hakutoka.
Ukiachana na hivyo, mara kadhaa, Rage
alijaribu kutaka kuwatoa wanachama walioonyesha kumpinga.
Wakati fulani Rage aliinuka na kucheza
kiduku hivyo kufanya ashangiliwe kwa nguvu na wanachama hao.
Pamoja na hivyo, Rage alifanikiwa
kuendesha kikao hicho kwa kujibu kibabe na kwa mkato maswali ya wanachama
waliokuwa wakimuuliza.
Pia suala la wanachama hao kupewa tiketi
za bure kuingilia katika mechi ya kirafiki kati ya Simba na URA iliyochezwa leo
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, kuliwafanya washangilie na kutotaka
kuchangia zaidi.
Watu waliokuwa kivutio katika kikao
hicho ni pamoja na mwenyekiti wa zamani wa Msimbazi, Hassan Dalali na Geofrey
Nyange ‘Kaburu’ ambaye alijiuzulu nafasi ya makamu mwenyekiti hivi karibuni.
0 COMMENTS:
Post a Comment