Ile kiu ya Wanayanga kumuona
mshambuliaji wao, Brendan Ogbu akiichezea timu hiyo kesho sasa haitakatwa.
Kiu hiyo haitakatwa kwa kuwa hatacheza
katika mechi ya kirafiki dhidi ya URA ya Uganda kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam.
Ogbu ameumia enka, hali inayomfanya
asicheze mechi hiyo na kuwanyima raha Wanayanga waliotaka kumuona.
Awali ilitangazwa kuwa Mnigeria huyo
atacheza mechi ya kesho, hivyo mashabiki wengi walitaka kumuona akiwa kazini.
Iwapo hatacheza kesho maana yake
atalazimika kusubiri hadi mechi nyingine ya kirafiki ambayo Yanga watacheza.
ayaaaaaaaaaaaaaa daaaaa
ReplyDelete