Beki wa Simba, Shomari Kapombe anaondoka
nchini leo kwenda Uholanzi kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la
kulipwa.
Kapombe anaondoka ikiwa ni baada ya TFF
kuridhia maombi yake ya kuondoka katika kikosi cha timu ya taifa na kwenda
kufanya majaribio.
Awali shirikisho hilo lilimzuia na kuharibu ratiba yake ya
majaribio hali iliyofanya wakala wake, Denis Kadito kulalama.
Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga
amethibitisha kuwa Kapombe atafanya majribio kwa siku hizo 14 akiwa nchini
humo.
Suala la timu anayofanya majaribio bado
halijawekwa wazi, ingawa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema
atajaribiwa FC Twente lakini wakala wake amekuwa akisisitiza suala hilo ni siri
na hajawahi kutaja ni timu gani atafanya majaribio zaidi ya nchi.







0 COMMENTS:
Post a Comment