| KIGGI (KUSHOTO) AKIMDHIBITI NGASSA WAKATI WAKIWA SIMBA PAMOJA.. |
Kiungo kinda wa Simba, Kiggi Makasi
ameamua kwenda kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kulitibu goti lake.
Rafiki wa karibu wa Kiggi, amesema kinda
huyo ameamua kufanya hivyo na mganga anayeaminika anaweza kumtibu yuko mjii
Bagamoyo.
“Kweli Kiggi ameamua kwenda kwa mganga
kwa kuwa amepania kurudi uwanjani, lakini mimi naona kama si kitu kizuri.
“Nimejaribu kumshauri lakini
imeshindikana kwa kuwa hata akibaki hawezi kupata matibabu na viongozi wa Simba
wamekuwa wagumu kupokea simu zake,” alisema rafiki huyo.
Alipoulizwa Kiggi kuhusiana na suala la
kwenda kwa mganga, hakutana kuzungumzia zaidi lakini akasema analazimika
kuhaika ili kupona na kurejea uwanjani.
“Lazima nihangaike ndugu yangu, nataka
kurudi uwanjani lakini masuala ya mganga tuachane nayo, kikubwa ninachotaka
kurejea ni uwanjani,” alisema.
Tayari Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden
Rage alisema mchezaji huyo atapatiwa matibabu kama ambavyo daktari bingwa
aliyeshauri apelekwe nchini India kwa ajili ya matibabu. Lakini hadi sasa
imekuwa kimya.







0 COMMENTS:
Post a Comment