Beki Mbuyi Twite ataikosa mechi ya
keshokutwa wakati Yanga itakapowavaa URA, timu inayomilikiwa na kampuni ya
watoza kodi ya mapato ya Uganda.
URA itakuwa nchini kucheza mechi mbili
za kirafiki, ikianza na Simba kesho kabla ya kuivaa Yanga, keshokutwa kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Twite amesema ataikosa mechi hiyo
kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti ingawa amekuwa akifanya mazoezi
taratibu.
“Kwa sasa niko kwenye usimamizi wa daktari
wa timu, naendelea kupata matibabu hivyo nimeona vizuri kama nitakaa nje ili
nipone vizuri,” alisema.
Awali Yanga ilikuwa icheze mechi ya
kirafiki dhidi ya 3 Pillars ya Nigeria, jana lakini ikagundulika timmu hiyo ilikuwa
bagumashi kupita kiasi.
TFF ikapoga stop mchezo huo kwa kuwa
Wanigeria hao walikuwa wameokotana lakini walitaka kucheza na mabingwa wa
Tanzania.







0 COMMENTS:
Post a Comment