| CHANONGO AKIWA KAZINI NA SIMBA... |
Kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Kim Poulsen ameamua kumhamisha namba kiungo wa pembeni wa Simba, Haruna Chanongo.
Poulsen raia wa Denmark amesema kutokana na kuwakosa Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu katika michuano ya Chan ameamua kumhamisha Chanongo.
“Chanongo anaweza kucheza namba ile, huenda atahitaji muda lakini huu ni wakati mwafaka.
“Kuna vitu alivyonavyo naona vinafaa kwa namba hiyo, ndiyo maana nikamuita kwa kazi hiyo na tayari tumeanza mazoezi katika hilo,” alisema Poulsen.
Chanongo amekuwa akitumika Simba kama winga wa kulia lakini hii itakuwa ni mara ya kwanza kucheza katikati wakati Taifa Stars itakapokuwa inaivaa Uganda katika mechi itakayopigwa Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuwania nafasi ya kucheza Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan).







0 COMMENTS:
Post a Comment